(1) Katika muda wa siku kumi na nne baada ya kutokea nafasi ya kazi katika afisi ya Naibu wa rais, Rais atamteua mtu mwingine kujaza nafasi hiyo, nalo Baraza la Kitaifa litapiga kura ya uamuzi wa uteuzi huo katika muda wa siku sitini baada ya kuupokea.
(2) Iwapo mtu atachukua mamlaka ya Naibu wa rais chini ya ibara ya (1), basi kwa kusudi la Kifungu cha 148 (8), mtu huyo atachukuliwa–
- (a) kama aliyehudumu kipindi chote cha Naibu wa rais, iwapo mnamo tarehe ya kuchukua mamlaka, zaidi ya miaka miwili na nusu inasalia kabla ya uchaguzi unaofuatia ulioratibiwa chini ya Kifungu 136 (2); au
- (b) hajahudumu katika kipindi cha afisi ya Naibu wa rais katika hali yoyote nyingine.