(1) Naibu wa rais anaweza kuondolewa mamlakani–
- (a) kwa misingi ya kutokuwa na uwezo wa kiakili na kimwili wa kutekeleza majukumu ya kiafisi;
- (b) kwa kura ya kutokuwa na imani–
- (i) kwa misingi ya kukosa uwezo wa kimwili na kiakili wa kutekeleza majukumu ya afisi;
- (ii) kwa sababu ya kuwa kuna sababu kubwa sana za kuamini kuwa Naibu Rais amefanya uhalifu wa jinai chini ya sheria za kitaifa ama kimataifa;
- (iii) kwa utovu mkubwa wa nidhamu.
(2) Sheria katika Vifungu vya 144 na 145 vinavyohusiana na kuondolewa mamlakani kwa Rais, kukiwa na mabadiliko yanayostahili, itatumika katika kumuondoa Naibu wa rais.