Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kuna afisi teule ya Katibu katika Baraza la Mawaziri ambayo ni afisi katika huduma za umma.

(2) Katibu katika Baraza la Mawaziri–

  • (a) atapendekezwa na Rais na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa kuteuliwa na Rais; na
  • (b) anaweza kuachishwa kazi na Rais.

(3) Katibu katika Baraza la Mawaziri–

  • (a) atakuwa na madaraka ya afisi ya Baraza la Mawaziri;
  • (b) atawajibika kulingana na maelekezo ya Baraza la Mawaziri, kwa kupanga shughuli na kuweka kumbukumbu za mikutano ya Baraza la Mawaziri;
  • (c) atawasilisha uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa watu au mamlaka zinazofaa; na
  • (d) atakuwa na majukumu kama itakavyoagizwa na Baraza la Mawaziri.

(4) Katibu katika Baraza la Mawaziri anaweza kujiuzulu kwa kutoa notisi ya maandishi kwa Rais.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-9/sehemu-3/kifungu-154/katibu-baraza-mawaziri/