(1) Kutabuniwa afisi ya Katibu Mkuu ambayo ni afisi katika huduma ya umma.
(2) Kila Wizara au idara ya Serikali itakuwa chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu.
(3) Rais–
- (a) atapendekeza mtu ili kuteuliwa kama Katibu Mkuu kutoka miongoni mwa wale waliopendekezwa na Tume ya Huduma za Umma; na
- (b) atamteua Katibu Mkuu kwa idhini ya Baraza la Kitaifa.
(4) Rais anaweza kubadilisha au kumhamisha kazi Katibu Mkuu.
(5) Katibu Mkuu anaweza kujiuzulu kwa kumuandikia Rais notisi