Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma anaweza kuachishwa kazi tu kwa misingi ya–

  • (a) kutoweza kutekeleza majukumu ya afisi kutokana na kukosa uwezo wa kiakili au wa kimwili;
  • (b) kutozingatia Sura ya Sita.
  • (c) kufilisika
  • (d) kutokuwa na umilisi.
  • (e) utovu wa nidhamu na tabia mbaya.

(2) Mtu anayetaka kuondolewa mamlakani kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Tume ya Huduma ya Umma ambayo, itakuwa kwa maandishi yakidhihirisha uhakika wa madai yanayounda msingi wa kuondolewa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma

(3) Tume ya Huduma ya Umma itaangalia malalamiko haya na, ikiridhika kwamba yanafichua kwa msingi wa malalamiko chini ya Ibara ya (1), itapeleka malalamiko haya kwa Rais.

(4) Baada ya kuyapokea na kuyachunguza malalamiko haya, Rais, kwa muda wa siku kumi na nne, atamsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ikisubiriwa uamuzi wa Rais kulingana na ibara ya (5) na atatekeleza haya kulingana na ushauri wa Tume ya Huduma ya Umma, atateua tume maalum itakayokuwa na–

  • (a) wanachama wanne kutoka miongoni mwa wale ambao wanashikilia au wameshawahi kushikilia afisi kama jaji wa mahakama yenye mamlaka makuu, au wale ambao wamehitimu kuweza kuteuliwa kwa afisi kama hii ;
  • (b) wakili mmoja ambaye amehudumu kwa angalau miaka kumi na mitano na atakayeteuliwa na taasisi ya kisheria inayowajibika kuthibiti taaluma ya uwakili; na
  • (c) watu wengine wawili walio na uzoefu wa masuala ya umma.

(5) Kamati itachunguza suala hilo kikamilifu na kuripoti kuhusu ukweli huo na kutoa mapendekezo kwa Rais ambaye atachukua hatua kulingana na mapendekezo hayo ya tume maalum.

(6) Mkurugezi wa Mashtaka ya Umma, ambaye amesimamishwa kazi kulingana na ibara ya (4) atapokea nusu ya mshahara hadi wakati wa kuachishwa kazi au kurudishwa kazini.

(7) Tume Maalum iliyoteuliwa kulingana na ibara ya (4) itamchagua mwenyekiti miongoni mwao.

(8) Tume Maalum iliyochaguliwa kulingana na ibara ya (4) itawajibika kuthibiti taratibu zake.

(9) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma anaweza kujiuzulu kwa kumuandikia barua Rais.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-9/sehemu-4/kifungu-158/kuondolewa-mkurugenzi-mashtaka/