Ruka hadi Yaliyomo

Katiba ya Kenya inazipa nguvu Serikali za Kaunti kukusanya mapato ya ndani ya kaunti. Kifungu cha 209 kinaeleza kuwa Serikali za Kaunti zinaweza kutoza ushuru kwa mali na kodi za burudani.

Mapato haya yanayokusanywa ndani ya kaunti ni mojawapo ya mapato ambayo serikali za kauti zinapata. Serikali za Kaunti huweka malengo (ya kifedha) ambayo zinatarajia kutimiza mwisho wa mwaka wa fedha.

Mwaka wa fedha (au mwaka wa bajeti) ni kipindi ambacho Serikali za Kaunti hutumia kwa madhumuni ya uhasibu, kupanga bajeti na kuripoti matumizi ya fedha.

Mwaka wa bajeti nchini Kenya unaanza tarehe 1 Julai mwaka tulio kwa sasa hadi tarehe 30 Juni ya mwaka ujao.

Msimamizi wa Bajeti hutoa ripoti jinsi Serikali za Kaunti zinavyotekeleza bajeti kila baada ya miezi minne na ripoti ya jumla kila mwisho wa mwaka. Ripoti hizi zinatokana na bajeti zilizoidhinishwa na Baraza la Kaunti na ripoti za fedha zinazowasilishwa na Serikali za Kaunti.

Ripoti hizo zinataarifiwa zaidi na data kutoka Mfumo wa Usimamizi wa Fedha (IFMIS).

Ripoti hizi huchambua, miongoni mwa mambo mengineo, juhudi za kila Serikali za Kaunti katika kukusanya mapato ya ndani ya kaunti. Tutaangaazia ripoti hizi za juhudi za Serikali za Kaunti katika kukusanya mapato katika makala haya.

Makala haya yatasasishwa mara kwa mara ili kuwezesha kutazamwa kwa juhudi za kaunti katika ukusanyaji wa mapato kwa miaka iliyopita na miaka ijayo.

Ripoti ziko katika muundo wa jedwali–

  • Lengo - ni lengo la kila mwaka la makadirio ya mapato ambayo kaunti ziliweka kukusanya mwishoni mwa mwaka wa kifedha;
  • Mapato - ni mapato halisi yaliyokusanywa mwishoni mwa mwaka wa fedha.
  • shilingi - ni shilingi za Kenya.
  • % - ni asilimia ya mapato halisi kama sehemu ya lengo la mwaka.

(Ikiwa jedwali halionekani kwa ukamilifu kwa simu ikiwa wima, geuza simu yako.)

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/mapato-ya-kaunti/